Raila akuje nyuma yako-Wavinya Ndeti amwambia Kalonzo

Muhtasari
  • Wavinya alibainisha kuwa sasa ni wakati wa Raila kupiga hatua moja nyuma na kumwacha Kalonzo Musyoka achukue udhibiti wa treni
GAVANA WA MACHAKOS WAVINYA NDETI
Image: TWITTER

Mkuu wa Kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti ametangaza kuwa taifa la Kamba halitamuunga mkono kiongozi wa ODM Raila Odinga iwapo hatajiuzulu na kumpendelea kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka.

Akizungumza katika Kaunti Ndogo ya Kathiani mnamo Jumanne Februari 14, Wavinya alibainisha kuwa sasa ni wakati wa Raila kupiga hatua moja nyuma na kumwacha Kalonzo Musyoka achukue udhibiti wa treni yao kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.

Hapa kuna watu sisi tume wa support kama jamii ya wakamba miaka mingi na wako na audacity ya kusimama wanasema ati mkamba ni nini. Hiyo madharau mtawacha, maneno ya kuona wakamba kama ghasia. Mkifanya siasa za Kenya, mkamba ako ndani ya map. Kwa hivo us kama kamba community, am telling H.E Mr Stephen Kalonzo Musyoka, sisi hatutaki kuchukuliwa madharau na mtu. Na wacha nikwambie sifichi sasa mheshimiwa Kalonzo Musyoka ambia Raila akuje nyuma yako. This time support H.E Kalonzo Musyoka and I am telling you with no fear of favour and if you do not him, we are not with you", Alizungumza Wavinya.

Wavinya alikuwa akijibu video ya mtandaoni iliyorekodiwa wakati wa Bunge la Wananchi Barazas, ambapo mfuasi mkali wa Raila Odinga Nuru Okanga alisikika akiwahutubia jamii ya Kamba.

Gavana huyo aliweka wazi kufanya kazi na serikali tawala kwa manufaa ya watu wa Machakos.