Mtaandamana mpaka mchoke-Rais Ruto amjibu Raila

Alisema atahakikisha katika wadhifa wake kama Rais hakuna mtu anayetishia Wakenya bila kuadhibiwa.

Muhtasari
  • Ruto alisema Kenya ni nchi ambayo itaendeshwa kwa misingi ya sheria na Katiba ambapo raia wote wana haki sawa
Ruto amjibu Odinga usiku
Ruto amjibu Odinga usiku
Image: Facebook

Rais William Ruto mnamo Jumatano, Februari 22, alimkashifu Kiongozi wa Azimio Raila Odinga kuhusu makataa yake ya siku 14.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tume ya Mto Nairobi (NRC) eneo la Korogocho, Kaunti ya Nairobi, Ruto alimuonya Raila dhidi ya kuanzisha ghasia nchini.

Mkuu wa nchi,ailishikilia kuwa hakuna mtu atakayeruhusiwa kumtisha yeye na serikali yake kwani Kenya ni ya kila mtu.

"Kwa hivyo hawa jamaa watulize boli. Ati wanataka kututisha na maandamo, watafanya maandano mpaka watachoka,"Mkuu wa Nchi amesema.

Katika Mkutano wa Kitaifa wa Maombi huko Jeewanjee Nairobi, Raila alitoa madai sita kwa Rais William Ruto, na kumwonya Mkuu wa Nchi kwamba atachukua hatua kali ikiwa atakosa kuchukua hatua.

Raila aliionya serikali ya Kenya Kwanza kwamba ataongoza nchi hiyo kwa hatua kubwa ya nchi nzima iwapo Rais Ruto atashindwa kuchukua hatua.

Ruto alisema Kenya ni nchi ambayo itaendeshwa kwa misingi ya sheria na Katiba ambapo raia wote wana haki sawa.

Alisema atahakikisha katika wadhifa wake kama Rais hakuna mtu anayetishia Wakenya bila kuadhibiwa.

"Kila mtu lazima aheshimu sheria na nchi hii inakwenda kuongozwa na sheria na tutahakikisha kuwa kila mtu anatii Katiba," alisema.