Waziri wa Utalii,Peninah Malonza abatilisha uteuzi wa Pauline Njoroge kama mwanachama wa bodi ya utalii

Pauline aliteuliwa na waziri wa zamani wa utalii Najib Balala

Muhtasari

• Ni mara ya pili uteuzi wa Pauline  umebatilishwa katika bodi ya utalii.

 Waziri wa Utalii,Peninah Malonza amebatilisha uteuzi wa Pauline Njoroge kama mjumbe wa bodi.

Njoroge aliteuliwa mwaka  2020 kuhudumu katika bodi ya utalii na aliyekuwa waziri wa Utalii Najib Balala. Hata hivyo siku ya Alhamisi Njoroge alikuwa miongoni mwa wanachama watano wa bodi hiyo waliopigwa kalamu na Malonza. 

Wengine ambao uteuzi wao ulibatilishwa ni Kevin Muasya, Najma Ismail, Alais Lenana Momoi na Isaac Muchiri Njangu.

Pauline Njoroge amekuwa kwenye mstari wa mbele kuishutumu serikali ya Kenya Kwanza.