Ichungw'a amjibu Raila baada ya madai alikuwa kwenye mkutano wa siri na DP Gachagua

Hivyo alitoa changamoto kwa Kiongozi wa Azimio la Umoja kushiriki ushahidi wa madai

Muhtasari
  • Mbunge huyo wa Kikuyu alijitenga na mkutano huo, ambapo Raila alidai kulikuwa na mipango ya kuwajeruhi zaidi ya wafuasi 1,000 wa Azimio la Umoja.
KIMANI ICHUNGW'A
Image: TWITTER

Kiongozi wa wengi katika Bunge la Kitaifa, Kimani Ichung'wah, Alhamisi, Machi 23, alijibu shutuma za Kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga za kupanga kuzua fujo kwenye maandamano ya Machi 27.

Alipokuwa akiongoza Bunge hilo, Ichung'wah alihudhuria kikao hicho na kutupilia mbali shutuma kali akibainisha kuwa Raila alikuwa akieneza uwongo dhidi yake.

Mbunge huyo wa Kikuyu alijitenga na mkutano huo, ambapo Raila alidai kulikuwa na mipango ya kuwajeruhi zaidi ya wafuasi 1,000 wa Azimio la Umoja.

 

"Nilitoka Bungeni kwa kuchelewa na kurudi nyumbani moja kwa moja. Mimi na binti yangu tulilala kwa kuchelewa na kuamka asubuhi na mapema, baada ya hapo nikaja moja kwa moja kazini," Ichung'wah alieleza.

Kulingana na Ichung'wah, Raila aliwazia matukio yasiyo na msingi na alihitaji kuthibitisha madai yake.

Hivyo alitoa changamoto kwa Kiongozi wa Azimio la Umoja kushiriki ushahidi wa madai ya kukutana na Naibu Rais Rigathi Gachagua na Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro.

"Bwana Odinga  unaweza kuwa hunijui vyema, unaeza kuwa unaota nakaribia jina lako la kati la "Mungu wa vurugu" tafadhali uliza mfadhili wako mimi ni mtu mwenye amani lakini  mwanamume wa mwisho wa kutishia na propaganda ,"Alisema Ichungw'a.