Rais Ruto na Raila Odinga wapongezwa kwa kukubali mazungumzo

Viongozi kadhaa nchini Kenya wamechukua hatua ya kuwapongeza Rais Ruto na Raila.

Muhtasari

•Viongozi hao walisema kuwa hatua hiyo ya viongozi hao itarudisha nchi katika utaratibu wa kikatiba.

•Odinga na Ruto walikubaliana kutumia bunge katika katika uteuzi wa makamishna wapya wa IEBC

Odinga amtambua Ruto kama rais
Odinga amtambua Ruto kama rais
Image: Facebook

Viongozi kadhaa nchini Kenya wamechukua hatua ya kuwapongeza Rais Ruto na Raila kwa kukubali kuingia katika mazungumzo.

Haya yanajiri baada ya Rais Ruto kumsihi Raila Odinga kusimamisha maandamano yaliyokuwa yamepangiwa Jumatatu akisema kuwa maandamano yamekuwa yakiathiri nchi kiuchumi na kusababisha uharibifu wa mali na vifo.

Kwa upande wake, Odinga alimjibu rais kwa kusema kuwa hatua ya rais ya kuhusisha bunge katika usajili  wa makamishna wapya wa IEBC ni nzuri na hivyo akasimamisha maandamano yaliyoratibiwa kufanyika.

Mashirika mbalimbali na baadhi ya viongozi na wamewapongeza wawili hao kwa hatua hiyo inayotarajiwa kuleta ustawi wa nchi.

Miongoni mwa viongozi hao ni Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru ambaye amesema kuwa anamshukuru Rais Ruto kwa kujizuia  na kurudisha nchi katika kuheshimu katiba na utulivu wa umma .

"Nampongeza Rais Ruto kwa kuonyesha sababu na kujidhibiti na pia kuirudisha nchi katika hali ya kuheshimu katiba na kuleta utulivu wa umma," alichapisha Waiguru.

Mutahi Ngunyi, mchambuzi wa masuala ya siasa pia amempongeza Rais kwa hatua hiyo ila akamuonya kumweka kando naibu wake Rigathi Gachagua katika mazungumzo yake ya siku za  usoni na Raila Odinga.

Gavana wa Nairobi, Johnson Sakaja akizungumza na The Star siku ya Jumatatu alisema kuwa busara ya Rais Ruto imeonyesha jukumu lake kama baba wa taifa.

"Namhongera Rais kwa busara yake na jukumu lake kama baba wa nchi. Lazima tuinuke kila wakati. Nina imani kuwa masuala yaliyoibuliwa na pande zote mbili yataleta hali ya usawa kwao wote," alisema Sakaja.

Shirika la IGAD kupitia Katibu mkuu,Workney Gebeheyu lilipongeza Ruto kwa kuonyesha utayari wao kufanya mazungumzo kusuluhisha tofauti zao kuusu masuala ya kitaifa kwa njia ya amani na kuhifadhi umoja wa Kenya na utaratibu  wa kikatiba.

"Nampongeza Rais William Ruto na Raila kwa utayari wao kushiriki katika mazungumzo kutatua tofauti zao kuhusu masuala ya kitaifa kwa njia ya amanina kuhifadhi umoja wa Kenya na utaratibu wa kikatiba," alisema.

Raila Odinga aliitisha maandamano tarehe 14 Februari, iliyoshudiwa na ghasia zilizoleta uharibifu wa mali na vifo. Odinga alidai kuwa Rais Ruto alikuwa amekosa kupunguza gharama ya maisha na pia alitaka kumshinikiza kufungua sava za za IEBC kwa madai ya wizi wa kura.

Kwa upande wake, Rais Ruto alidai kuwa hatua ya Raila Odinga ilikuwa ya kuficha ajenda zake za kibinafsi za kutaka kuwa serikalini kwa kuibua madai hayo ya wizi wa kura na gharama ya maisha.