Dhehebu la Shakahola: Serikali kupanua msako wa miili hadi mbuga ya Tsavo

Miili zaidi ya 230, tayari imefukuliwa na idadi ya miili zaidi inatarajiwa kufukuliwa.

Muhtasari

•Kindiki amesema kuwa serikali itatumia droni kusaidia juhudi za wachunguzi wanaofanya msako wa miili ardhini.

Image: BBC

Msako wa wa manusura na miili ya watu waliokufa kutokana na mfungo katika dhehebu ‘tata’ la msitu wa Shakahola , Kilifi nchini Kenya utapanuliwa hadi katika Mbuga ya Wanyama ya taifa ya Tsavo East, Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Kithure Kindiki , amenukuliwa na vyombo vya habari Jumamosi akisema.

Amesema kuwa serikali itatumia droni kusaidia juhudi za wachunguzi wanaofanya msako wa miili ardhini huku mchakato wa kufukua miili katika makaburi ya pamoja uliwa umesimamishwa ili kuruhusu uchunguzi wa maiti ufanyike .

"Msako wa manusura na miilindani yam situ wa Shakahola na katikaChakama Ranch kwa ujumla utaendelea bila kuvurugwa na utapanuliwa hadi ndani ya mbuga ya Wanyama ya taifa-Tsavo East National Park katika siku zijazo kwa msako wa ardhini na wa anga kwa kutumia droni," alisema wazir Kindiki katika taarifa yake.

Ijumaa watu zaidi waliokolewa katika msitu wa Shakahola, na hivyo kupelekea idadi ya watu waliookolewa katika tukio ambapo mchungaji Paul Mackenzie Nthenge wa kanisa la Good News International aliripotiwa kuwaagiza wafuasi wake kufunga hadi kufa ili ‘’kukutana na Yesu’’ kufikia 90.

Miili zaidi ya 230, tayari imefukuliwa na idadi ya miili zaidi inatarajiwa kufukuliwa, kulingana na maafisa.

Shughuli ua kufukua miili ilisitishwa Alhamisi ili kutoa fursa ya uchunguzi wa miili , na inatarajiwa kuanza tena Jumatano wiki ijayo.