BIASHARA HARAMU

Pembe za ndovu zanaswa, mmoja akamatwa DCI - Laikipia

Zina uzani wa zaidi ya kilo 110 na thamani ya mamilioni ya pesa

Muhtasari

• Pembe za ndovu zenye thamani ya mamilioni ya pesa zimenaswa kwa mujibu wa idara ya upelelezi nchini DCI.

• Idara hiyo inakiri kuwa,pembe hizo zenye uzani wa zaidi kilo 110 zimepatikana katika kaunti ya Laikipia huku mshukiwa mmoja aliyetambuliwa kama Alfred Gathecha akikamatwa.

 

Pembe za ndovu zenye thamani ya mamilioni ya pesa zimenaswa kwa mujibu wa idara ya upelelezi nchini DCI.

Idara hiyo inakiri kuwa,pembe hizo zenye uzani wa zaidi kilo 110 zimepatikana katika kaunti ya Laikipia huku mshukiwa mmoja aliyetambuliwa kama Alfred Gathecha akikamatwa.

Katika uchunguzi ulioongozwa na wachunguzi kutoka idara hiyo, kitengo hatari cha kufanikisha uchunguzi,mwaume huyo mwenye umri wa miaka 47 alitiwa nguvuni katika eneo la Sipili  kata ya Kirima baada ya gari lililokuwa likisafirisha pembe hizo kusimamishwa.

Walipokuwa wakijifanya kama wanabiashara wa visima vya mafuta, maafisa hao walimvuta mshukiwa kabla ya kumweka pingu muda mchache kabla ya saa saba adhuhuri hapo jana.

Mshukiwa atakuwa akifikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuendeleza na kuwahatarisha wanyamapori kwa mujibu wa sheria kipengele cha 92(2) kitengo cha utunzaji na kuhifadhi wanyamapori cha 2013.

Pembe za ndovu  huwa na faida katika soko haramu kwa maana  zinaendelea kuhitajika  katika mkoa wa Mashariki ambao huendeleza biashara hiyo nharamu hasa kutoka Afrika. Raia wanashauriwa kuendelea kujitokeza kuwasilisha ujumbe hasa kuhususiana na kuwindwa kwa wanyamapori  katika idara ya upelezi DCI .