MAINA NJENGA AZUILIWA

Polisi watawanya wafuasi wa Maina Njenga katika makao ya DCI

Waandamanaji wa Maina Njenga watimuliwa kutumia vitoa machozi

Muhtasari

•Polisi wamelazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika makao ya DCI yaliyopo barabara ya Kiambu Alhamisi 25.

Polisi wamelazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika makao ya DCI yaliyopo barabara ya Kiambu Alhamisi 25.

Watu hao wanaoaminiwa kuwa wafuasi wa Maina Njenga,walivamia makao hayo ya idara ya upelelezi ili kudai kuachiliwa kwa kiongozi wao ambaye bado alikuwa amezuiliwa akihojiwa.

 

Njenga mwenyewe alijiwasilisha  kwa maafisa wa polisi mjini Nakuru mnamo Mei 24, kuhojiwa.

Kiongozi huyo wa awali wa kundi la Mungiki amekuwa akizuiliwa katika makao hayo ya idara ya upelelezi  huku akihojiwa kuhusiana na madai ya  kupatikana kwa bunduki mbili pamoja na misokoto 90 ya bangi iliyopatikana katika makao yanayohusishwa naye  eneo la Ngomongo kata ya Bahati.