Martha Karua amchana vibaya Gachagua kwa kumwambia Wajackoyah asiende Mlima Kenya

Rigathi Gachagua, alidokeza kuwa ilikuwa makosa kumpeleka Wajackoya katika eneo la Mlima Kenya

Muhtasari
  • Naibu Rais aliwataka viongozi wa Mlima Kenya katika Muungano wa Azimio waache kupunguza vita vyao vilivyoboreshwa na serikali kuhusu matumizi mabaya ya dawa za kulevya

Martha Karua kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa twitter amemkosoa na kumchana naibu Rais Gachagua kwa kuwasuta viongozi wanaompeleke kiongozi wa chama cha Roots Wajackoyah mlima Kenya.

Rigathi Gachagua, alidokeza kuwa ilikuwa makosa kumpeleka Wajackoya katika eneo la Mlima Kenya kwa vile anaunga mkono kuhalalishwa wa bangi.

Naibu Rais Rigathi Gachagua alitoa maoni haya wakati ambapo taifa lilikuwa limeanza kampeni dhidi ya utumizi mbaya wa dawa za kulevya na pombe.

"Kinachotia aibu ni matamshi na mienendo ya wahusika kama yeye ambao wana masuala makubwa ya uadilifu ambayo hayajatatuliwa, na ambao wana tabia kama wakorofi wa kijijini."

Aliwakashifu haswa viongozi wa Mlima Kenya ambao ni washirika wa muungano unaoongozwa na Raila Odinga akisema wanarejesha nyuma juhudi za serikali kumaliza janga la dawa za kulevya katika eneo la kati.

“Viongozi wetu wa Mlima Kenya wanajua jinsi ambavyo tumetatizwa na pombe na bangi. Na viongozi wetu wa Mlima Kenya huko Azimio mgeni rasmi ni Wajackoyah wanapozuru,” akasema.

"Wanajaribu kuwaambia nini watoto wetu, huyu ni mtu ambaye alisema kwenye televisheni ya taifa kwamba bangi haipaswi tu kuvutwa bali alihimiza watu kuikuza."

Naibu Rais aliwataka viongozi wa Mlima Kenya katika Muungano wa Azimio waache kupunguza vita vyao vilivyoboreshwa na serikali kuhusu matumizi mabaya ya dawa za kulevya na vileo katika eneo la Kati kwa kukataa kumshirikisha katika ziara zao katika eneo hilo.

“Nataka kuwauliza viongozi mkija hapa mje mzungumze mambo yenu lakini msije na Wajackoyah. Kwani unatuambia nini hapa? Unatudharau kwa kiasi gani? Unapoleta Wajackoyah hapa, unatucheka tu,” alisema.

Gachagua ameapa kuwa msako mkali dhidi ya pombe haramu na utumizi wa dawa za kulevya ambao umeangamiza maelfu ya vijana.

Gachagua alisema haitakuwa biashara kama kawaida na ameviagiza vikosi vya usalama kufanya msako mkali dhidi ya mashimo ya pombe haramu na kuwabaini walanguzi wa dawa za kulevya ambao wana nia ya kuwaangamiza vijana na watoto wa Kenya.