DP Gachagua ajitolea kumsaidia Faith Kipyegon kuwekeza mapato yake

Waziri huyo alikariri kuwa serikali itakuwa na mpango wa zawadi na mwongozo wa jinsi ya kuwatuza wanariadha wa Kenya

Muhtasari
  • Serikali limemzawadia Kipyegon Ksh.5 milioni kwa rekodi moja na nyumba ya Ksh.6 milioni kwa rekodi nyingine.
Naibu wa rais amefichua sababu za kutolitumia jina lake la ubatizo.
Naibu wa rais amefichua sababu za kutolitumia jina lake la ubatizo.
Image: Facebook

Naibu Rais Rigathi Gachagua amewataka wanariadha wa Kenya kuwekeza mapato yao kwa busara, ili kuepuka machungu baada ya kustaafu.

Akizungumza katika Ikulu siku ya Jumanne, wakati wa hafla ya kuwakaribisha walioshikilia rekodi ya dunia Faith Kipyegon na Ferdinand Omanyala, Gachagua aliwapongeza wanariadha hao kwa kuiweka Kenya kwenye ramani ya dunia.

“Inasikitisha tunapoona watu ambao wamefanikiwa sana na maarufu wanaishi katika umaskini baada ya kustaafu. Ninataka kumwalika Faith...Omanyala kutafuta njia za kuwekeza,” Gachagua alisema.

Naibu Rais aliendelea kumtaka Kipyegon, ambaye sasa anashikilia Rekodi za Dunia za mita 1500 na 5000 kumfikia ikiwa atahitaji vidokezo vya uwekezaji.

"Faith, iwapo utakuwa na tatizo la kujua namna gani unaweza kuwekeza chochote unachokwenda kukipata, mimi ninapatikana, mimi ni mfanyabiashara makini sana, naweza kukuongoza ili kuhakikisha unafanikiwa," alisema.

Serikali limemzawadia Kipyegon Ksh.5 milioni kwa rekodi moja na nyumba ya Ksh.6 milioni kwa rekodi nyingine.

Alieleza kusikitishwa na hali ya kusikitisha ya baadhi ya wanariadha mashuhuri na waliofanikiwa kuishi katika tabu na umaskini baada ya kustaafu.

Katika hafla hiyo, wawaziri wa Michezo, Sanaa na Vijana Ababu Namwamba alimshukuru rais kwa msaada kwa idara ya michezo na sanaa.

"Ninataka kukushukuru kwa usaidizi thabiti wa usawa ambao umetangaza kwa michezo na wabunifu," alisema Namwamba.

Haya yanajiri baada ya rais kuzindua mpango wa Talanta hela, unaolenga kutambua, kuajiri, kukuza, soko na kuchuma talanta.

Waziri huyo alikariri kuwa serikali itakuwa na mpango wa zawadi na mwongozo wa jinsi ya kuwatuza wanariadha wa Kenya watakaovunja rekodi ya dunia kwa kuhifadhi mafanikio ya kimataifa au kikanda.