Kindiki atangaza Jumatano sikukuu ya kuadhimisha Eid-ul-Adha

Kindiki alibainisha tangazo hilo katika notisi ya gazeti la serikali iliyotolewa siku ya Jumatatu mchana.

Muhtasari

• Kindiki alibainisha tangazo hilo katika notisi ya gazeti la serikali iliyotolewa siku ya Jumatatu mchana.

KITHURE KINDIKI AKIWA MBELE YA KAMATI YA USAILI YA BUNGE LA KITAIFA
Image: EZEKIEL AMINGA

Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ametangaza Juni 28, 2023 kuwa sikukuu ya sherehe kuadhimisha Eid-Ul-Adha.

Kindiki alibainisha tangazo hilo katika notisi ya gazeti la serikali iliyotolewa siku ya Jumatatu mchana.

“Inajulishwa kwa taarifa ya jumla kwa umma kwamba kwa kutekeleza mamlaka aliyopewa na kifungu cha 2 (2) na sehemu ya II ya schedule, kama inavyosomwa na kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Umma, waziri wa usalama ya Ndani na Utawala wa Kitaifa inatangaza kwamba Jumatano, tarehe 28 Juni, 2023, itakuwa siku kuu ya kuadhimisha Eid-Ul-Adha (Idd-Ul-Azha)," notisi hiyo ilisoma.

Katika sherehe hizi za Eid al-Adha, Waislamu huonyesha utiifu wao kwa Mwenyezi Mungu kwa kutoa kafara ya mnyama. Sikuu hiyocimetokana na hadithi kutoka kwa Quran ambayo pia inajulikana kwa Wakristo na Wayahudi.

Sikukuu hii huadhimishwa kote ulimwenguni kwa ndugu zetu waislamu kama ukumbusho wa nia ya Nabii Ibrahimu kujitolea kila kitu kwa ajili ya Mungu.

Eid al-Adha ni siku ya 10 ya Dhu al-Hijjah, mwezi wa kumi na mbili na wa mwisho katika kalenda ya Kiislamu.

Kwa kuwa siku kamili inategemea kuonekana kwa mwezi, tarehe inaweza kutofautiana kati ya nchi kwa nyingine.