Hatutalipa ushuru kwa serikali ya Kenya Kwanza - Azimio

"Kuanzia leo tunaanza kampeni ya ukaidi na uasi wa raia kwa serikali... ikiwa ni pamoja na kukataa kulipa kodi," alisema Eugine Wamalwa.

Muhtasari

• Eugine Wamalwa alibainisha kuwa muungano wa Azimio sasa ulilazimika kutoa wito kwa wafuasi wake kukataa kulipa kodi kama njia moja ya kuwilazimisha serikali kujiondoa usukani.

Viongozi wa Azimio wakiongozwa na Raila Odinga.
Viongozi wa Azimio wakiongozwa na Raila Odinga.
Image: SCREENGRAB

Aliyekuwa waziri wa ulinzi na kiongozi wa chama cha DAP-K  Eugine Wamalwa amesema kwa sasa upande wa upinzani unawahimiza wafuasi wake kutolipa ushuru kwa serikali.

Eugine akizungumza katika mkutano wa muungano wa Azimio, alisema kuwa serikali ya Kenya Kwanza iliazimia kuwadhulumu na kuwanyanyasa Wakenya ambao waliwachagua viongozi hawa.

Eugine Wamalwa alibainisha kuwa muungano wa Azimio sasa ulilazimika kutoa wito kwa wafuasi wake kukataa kulipa kodi kama njia moja ya kuwilazimisha serikali kujiondoa usukani.

"Kuanzia leo tunaanza kampeni ya ukaidi na uasi wa raia kwa serikali... ikiwa ni pamoja na kukataa kulipa kodi ambayo lengo lake ni kumlazimisha Rais Rutona serikali yake kwenda nyumbani." alisema Eugine Wamalwa.

Muungano wa azimio sasa unasema kuwa hakuna mazungumzo ya pande mbili baina yao na upande wa serikali umsefutiliwa mbali rasmi na sasa wanaingia maandamano.

"Hakuna mazungumzo tena! kwa hivyo baada ya kutuwekea vikwazo vya ushuru vya adhabu kali vilivyo katika  sheria ya fedha ya 2023, bila kujali maoni yetu kabisa. Tunatangaza kumalizika kwa mazungumzo ya pande mbili tulizotuma wajumbe wetu... ni wakati wa kuchukua hatua. wakati wa kuongea umekwisha sasa ni action."

Eugine Wamalwa pia wataungana siku ya Saba Saba, tarehe Julai 7 mwaka huu ili kuainisha mipango ya

"Sisi wote wananchi tutakutana siku ya saba ya mwezi Julai 2023 siku ya saba saba, tukio ambalo litafungua mpango wa kutotii serikali ili kurudisha serikali hii ya Kenya Kwanza  nyumbani."