Fahamu kaunti ambazo wanaume walishiriki ngono mara ya kwanza na umri wa chini kabisa

West Pokot inaongoza kwa umri wa chini kabisa ambapo wanaume walifanya mapenzi kwa mara ya kwanza.

Muhtasari

• Utafiti unaonyesha wanaume wa West Pokot walishiriki tendo la ndoa kwa mara ya kwanza wakiwa na umri wa wastani wa miaka 15.4.

•Mandera (miaka 24.9) inaongoza kwa umri wa wastani wa juu zaidi ambapo wanaume walifanya mapenzi kwa mara ya kwanza nchini Kenya 

Image: GETTY IMAGES

Kaunti ya West Pokot inaongoza kwa umri wa wastani wa chini kabisa ambapo wanaume walifanya mapenzi kwa mara ya kwanza nchini Kenya.

Utafiti wa Demografia na Afya ya Kenya 2022 (KDHS 2022) uliofanywa na KNBS unaonyesha kuwa wanaume katika kaunti hiyo ya mkoa wa bonde la ufa walishiriki tendo la ndoa kwa mara ya kwanza wakiwa na umri wa wastani wa miaka 15.4.

Kaunti ya Kericho inafuatia kwa umri wa wastani wa chini kabisa ambapo wanaume walifanya ngono kwa mara ya kwanza, miaka 15.7.

Utafiti huo ulifanywa kwa wanaume wenye umri wa miaka 25 hadi 54.

Kaunti ya Machakos (miaka 15.7) imeorodheshwa kama kaunti ya tatu kwa umri wa wastani wa chini kabisa ambapo wanaume walipata uzoefu wao wa kwanza wa mapenzi, ikifuatiwa na Nakuru (miaka 15.7 na Tharaka Nithi (miaka 15.7).

Kwa upande mwingine, Kaunti ya Mandera inaongoza kwa umri wa wastani wa juu zaidi ambapo wanaume walifanya mapenzi kwa mara ya kwanza nchini Kenya huku wanaume wakishiriki tendo hilo kwa mara ya kwanza wakiwa na umri wa miaka 24.9.

Wajir ameorodheshwa ya pili kwa umri wa wastani wa juu zaidi ambapo wanaume walifanya ngono kwa mara ya kwanza, wakiwa na miaka 22.4. Garissa anafuata akiwa na umri wa wastani wa miaka 22.3 na Kirinyaga akiwa na umri wa wastani wa miaka 22.1.