Narok yaongoza kwa wanawake ambao wameshiriki tendo la ndoa mara nyingi kwa wiki 4

Kulingana na ripoti ya utafiti huo, asimia 48.4 ya wanawake nchini wameshirki katika tendo la ndoa katika wiki nne zilizopita huku asilimia 15.4 pekee wakiwa hawajawai fanya mapenzi.

Muhtasari

• Wanawake kwenye kaunti ya Marsabit, Vihiga na Wajir ni miongoni ya kauti zilizovuta mkia kati ya wanawake hao waliojamiana hivi majuzi kabisa kwa asilimia 30.3, 35.4 na 37.0 mtawalia.

Image: GETTY IMAGES

Utafiti mpya uliotolewa na KNBS umeonyesha kwamba wanawake wengi katika kaunti ya Narok, Embu na Murang’a nchini wameshiriki tendo la ndoa hivi majuzi zaidi.

Kulingana na ripoti ya utafiti huo, asilimia 48.4 ya wanawake nchini wameshiriki katika tendo la ndoa katika wiki nne zilizopita huku asilimia 15.4 pekee wakiwa hawajawai kufanya mapenzi.

Pia wanawake asilimia 24.9 ya wanawake nchini wamewai shiriki katika ngono chini ya mwaka mmoja uliopita na wengine asilimia 11.2 wakiwa wamefanya tendo hilo kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

“Asilimia ya usambazaji wa wanawake wenye umri wa miaka 15-49 kwa muda wa kujamiiana mara ya mwisho, kulingana na kaunti tafauti tofauti nchini. Kati ya wanawake 16,716 walishirikishwa katika utafiti huu, wanawake asilimia 48.4 wameshiriki tendo la ndoa ndani ya wiki nne zilizopita.”

Wanawake kwenye kaunti ya Marsabit, Vihiga na Wajir ni miongoni ya kauti zilizovuta mkia kati ya wanawake hao waliojamiiana hivi majuzi kabisa kwa asilimia 30.3, 35.4 na 37.0 mtawalia.

Wanawake katika kaunti ya Nairobi ilikuwa na wanawake wengi zaidi walioshirikishwa katika utafiti huo, ilikuwa kati ya kaunti 15 bora na asilimia 47.9.

Katika ripoti hiyo iliyowashirkisha wanawake kati ya umri ya miaka 15 na 49, wanawake katika kaunti ya Wajir iliongoza kwa wanawake ambao hawajawi kushirki ngono maishani mwao.

Baadhi ya kauti zingine nchini katika utafiti huu: Mombasa asilimia 42.6, Machakos 49.6, Nyeri 50.8, Nakuru 51.5 na  Kisii 50.2.