Wamuratha ataka wanawake wa Limuru waliolazimishwa kuvua nguo walipwe fidia

Polisi walisema wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani siku ya Ijumaa kujibu mashtaka mbalimbali.

Muhtasari
  • Akizungumzia tukio hilo ambalo limezua hisia tofauti kutoka kwa wananchi, Wamuratha alizidi kuwataka viongozi wanawake wote Bungeni kujitokeza kupigania haki ya wanawake walioathirika.

Mwakilishi wa Wanawake wa Kiambu Ann Wamuratha sasa anataka wanawake walioathiriwa na kitendo kinachodaiwa kufanywa na kampuni ya Limuru kulipwa fidia.

Akizungumzia tukio hilo ambalo limezua hisia tofauti kutoka kwa wananchi, Wamuratha alizidi kuwataka viongozi wanawake wote Bungeni kujitokeza kupigania haki ya wanawake walioathirika.

“Kama Mwakilishi wa Wanawake wa Kiambu, ninalaani kwa maneno makali iwezekanavyo. Hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya kampuni ili iwe fundisho kwa kila mtu na ikiwezekana wawafidie wanawake hao kwa kuwadharau,” alisema.

Huwezi kufanya hivyo kwa binadamu mwenzako; kwamba uwafungie kwenye chumba ili kuthibitisha kama wako kwenye siku zao ili kubaini kama wao ndio walioondoa taulo za usafi,” aliongeza.

Kizaazaa ambacho wafanyikazi wa kike wa kampuni ya Limuru walilazimishwa kuvua nguo wakiwa kazini kimepelekea mameneja watatu kukamatwa.

Wafanyikazi hao walilalamika kuwa wamelazimishwa kuvua nguo.

Mameneja watatu wakuu katika kampuni hiyo walikamatwa siku ya Alhamisi kuhusiana na kisa hicho ambapo wafanyikazi hao wa kike walidaiwa kulazimishwa kuvua nguo wakiwa kazini.

Polisi walisema wafanyakazi hao wa kike walilazimishwa kuvua nguo na meneja aliyetaka kujua ni nani alikuwa amevua taulo kwenye pipa lisilofaa.

Waliokamatwa ni pamoja na Meneja Uhakikisho wa Ubora wa kiwanda, Meneja Rasilimali Watu, na Msaidizi wa Utumishi, polisi walisema.

Polisi walisema wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani siku ya Ijumaa kujibu mashtaka mbalimbali.