Hata muandamane, hakuna nusu mkate - Ndindi Nyoro

"Waandamane juu ya mti, waandamane juu ya nyumba hatutawapa serikali ya nusu mkate.” Ndidi Nyoro alisema.

Muhtasari

• Ndindi Nyoro amesema kuwa hata muungano wa Azimio waandamane juu ya mti na hata kwenye barabara hawatarahusu kuingia katika serikali ya mgao.

• Kauli za Nyoro zilikuja saa chache tu baada ya Rais Ruto kujitokeza huku akijipiga kifua na kutoa amri kuwa hataruhusu maandamano hayo kufanyika tena.

nyoro
nyoro

Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro amewahakikishia upande wa upinzani wanaoandaa maandamano kwa sababu ya gharama ya juu ya maisha kuwa hawatakubali kuwe na serikali ya nusu mkate.

Mbunge huyo anayehudumu muhula wa pili katika bunge la kitaifa amesema kuwa hata muungano wa Azimio uandamane juu ya mti na hata kwenye barabara hawatarahusu kuingia katika serikali ya mgao.

“Ati wanafikiria sisi ni waoga, wanatutishia na maandamano hapa na maandamano pale. Wakienda kwa uchaguzi wanashindwa sasa wanafikiria wataingia katika serikali kwa njia ya mkato. Nataka niwaambie na wasikie vizuri. Waandamane juu ya mti, waandamane juu ya nyumba hatutawapa serikali ya nusu mkate.”

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Bunge kuhusu Bajeti, alionya kuwa hawataruhusu maandamano hayo kufanyika katika eneo la mlima Kenya.

Kulingana na Nyoro waandamanaji hao walikuwa majambazi waliokombolewa kuleta vurugu kwa biashara zao.

Semi za Nyoro zilikuja saa chache tu baada ya Rais Ruto kujitokeza na kutoa amri kuwa hataruhusu maandamano hayo kufanyika tena.

Ruto ameeleza kuwa ni kutokana na maandamano ya siku zilizopita ambapo watu waliaga dunia na wengine kupata majeraha mabaya huku mali yasiyokadirika yakiharibiwa na waandamanaji, ambapo alisema huwa hataruhusu hilo liendelee tena.

Mliona juzi, walifanya maandamano Ijumaa iliyopita ile ingine watu saba wakakufa, wamefanya maandamano juzi watu nane wamekufa. Mimi nataka niwaulize, mnataka tuendelee na hii maandamano? Mnataka tuendelee na hii maandamano? Mimi nataka niwaambie, maandamano haiwezi kufanyika tena katika taifa la Kenya,”  Aliuliza Ruto.

Matamshi haya ya viongozi wa upande wa serikali unajuabaada ya muungano wa Azimio kutangaza kuwa sasa wamepanga maandamano ya wiki ijayo itafanyika siku tatu kuanzia Jumatano hadi Ijumaa.