Mama amuua mwanamume kwa madai ya kumnajisi binti yake wa miaka 2

Baada ya kumuua mwanaume huyo wakazi wa kijiji hicho walimvamia nakumjeruhi vibaya mwanamke huyo anayefahamika kama Cheptoo.

Muhtasari

• Mwanamke huyo alikiri kumuua mwanaume huyo kwa chifu wa eneo lake baada ya kudai kuwa mwanume huyo alimbaka mtoto wake wa miaka 2.

• Nyumba ya mwanamke huyo iliteketezwa baada ya mwanamke huyo kuokolewa.

Crime scene
Crime scene
Image: HISANI

Mwanamke mmoja kutoka kijiji cha Kolong eneo bunge la Emgwen, Kaunti ya Nandi siku ya Alhamisi alidaiwa kumuua mwanamume kwa madai ya kumnajisi bintiye wa miaka miwili.

Polisi wa kituo cha Kamombo Patrol Base walisikia kisa hicho kwanza kutoka kwa chifu wa eneo hilo ambaye aliripoti kuwa mwanamke huyo, aliyejulikana tu kama Cheptoo, alikiri kumuua mwanaume huyo kwa simu.

Maafisa wa Kamombo walipofika katika eneo la tukio, walizuiliwa kuingia katika eneo hilo na umati wenye hasira ambao ulikuwa kumshambulia Cheptoo.

"Walitaka kumuua Cheptoo. Maafisa hao kutoka Kamombo waliitisha msaada kutoka kwa wenzao wa Kituo cha Polisi cha Kapsabet," Kamanda wa Polisi wa gatuzi Ndogo ya Nandi, David Anyir alisema.

David aliongeza: "Maafisa wa ziada kutoka Kapsabet walikimbia hadi eneo la tukio kuwapa nguvu zaidi na kufanikiwa kumuokoa mwanamke huyo."

 

Aliongeza kuwa nyumba ya mwanamke huyo iliteketezwa baada ya mwanamke huyo kuokolewa.

Cheptoo alipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Kapsabet ambapo anapokea matibabu.