Hakuna aliye na mamalaka ya kukomesha maandamano - Azimio

Tuanafanya maandamano yetu kwa mujibu wa katiba, hakuna wa kukinzana nayo - Wandayi

Muhtasari

•Serikali ya Kenya Kwanza iliapa kukabiliana na waandamanaji, ambapo waziri wa usalama alitoa amri kwa maafisa wa usalama kuwa tayari Jumatano wiki hii.

Image: Viongozi wa Azimio la Umoja// TWITTER

Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya umeapa kuendeleza kalenda ya maandamano yao ya amani taifa zima kama walivyopanga na kuratibiwa hapo awali.

Katika kikao chao Jumatatu 17, kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa Opiyo Wandayi amekiri kuwa hakuna mtu yeyote nchini ambaye ana mamlaka ya kusitisha au kukomesha maandamano yanayopangwa na mtu au kikosi cha watu nchini.

Wandayi alisema kuwa, licha ya kupokea vitisho vikali kutoka kwa viongozi wa serikali wakiwemo Rais Ruto, waziri wa usalama Kithure na Kindiki na naibu Rais Righathi Gachagua, maandmano yao ya siku tatu yangali yapo.

Maandamano ya amani yaliyopangwa Jumatano, Alhamisi na Ijumaa juma hili yatafanyika kama yalivyopangwa na kuamuliwa na viongozi wetu. Hili litafanyika kulingana na kipengele 37 cha katiba ya nchi, Tunapaswa kama sote tunavyofahamu kuwa tunao uhuru wa kufanya mikutano ya amani. Hakuna yeyote anapaswa kukinzana na kipengele hicho,” Alisema Wandayi.

Azimio walisema kuwa mpango wa ukusanyaji wa saini za kutosha kuibandua serikali ya Kenya Kwanza mamlakani ungali unaendelea, ambapo viongozi hao walitoa taarifa wakisema kuwa pia hilo wanalifanya kulingana na kipengele 1 cha katiba, ambacho kinasema kuwa uongozi na mamlaka ya taifa ni kulingana na wananchi, na hivyo uongozi ni wananchi.

Haya yanajiri wakati ambapo Rais William Ruto aliapa kuwa hataruhusu maandamano tena nchini, ambapo alisema kuwa maandamano yanayopangwa na viongozi wa upinzani yanalenga kuyavuruga maendeleo ya taifa na hivyo hataruhusu yafanyike.

Kauli kama ya Rais, imeungwa mkono na waziri wa usalama nchini Kithure Kindiki, ambaye pia alisema yuko tayari kukabiliana na waandamanaji siku hiyo ikifika akitoa amri kwa maafisa wa usalama nchini kuwa tayari.