Mbunge Peter Salasya amtishia waziri Moses Kuria baada ya kauli tata

"Kako na mdomo na hakana nguvu. Wednesday tupatane tupigane tu mangumi na nitakutandika.” Peter Salsasya alisema.

Muhtasari

• Mbunge Peter Salsya alisema kuwa ataelekeza nguvu zake kwa waziri Moses Kuria wakati wa maandamano ya upinzani siku ya Jumatano.

• Peter Salasya amejitokeza baada ya waziri Kuria kuchapisha jumbe mitandaoni akiashiria mipango ya kumuua mtu ambaye hakumtambulisha.

Mbunge wa Mumias Mashariki na Waziri Moses Kuria.
Mbunge wa Mumias Mashariki na Waziri Moses Kuria.

Mbunge wa Mumias East, Peter Salasya ametangaza wazi kuwa mnamo siku ya Jumatano, wakati wa maandamano ya Azimio, yeye atashughulika na kukabiliana na waziri wa Biashara na viwanda, Moses Kuria.

Huku akionyesha kughadhabishwa na ujumbe wa waziri huyo kwenye akaunti yake ya twitter, Salasya alieleza kuwa yeye ataangazia nguvu zake kwa waziri huyo akidai alikuwa akizungumza sana na hana nguvu.

“Mimi Wednesday, maandamano yangu ni kutandikana na Moses Kuria. Kako na mdomo na hakana nguvu. Wednesday tupatane tupigane tu mangumi na nitakutandika.”

Aliendeleza mashambulizi yake kwa waziri huyo akisema kuwa hawatamruhusu aendelee kutishia kumuua kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

“Hatutaruhusu uendelee kumtishia kiongozi wetu na snipers. Kila mtu atakufa tu na si ati wewe huwezi kufa, sisi wote ipo siku tutaondoka duniani.”

Waziri Kuria katika misuru ya jumbe katika akaunti yake rasmi ya Twitter, alionekana kuashirikia kupanga kifo cha mtu mmoja ambaye hakufichua jina lakini wanamitandao walionekana kufikiria jumbe hizo za Kuria zilimlenga kiongozi wa muungano wa Azimio Raila Odinga.

Moja ya jumbe hizo zilisoma, “Atakufa Wednesday 19 azikwe Saturday 29th. Jowi.”

Ujumbe mwingine uliochapishwa siku ya Jumamosi ulisema kuwa hawangeruhusu mtu huyo kuingia katika salamu na Rais kwa kuwa alihisi yeye na watu waliompigia Rais kura wataachwa mataani.

Saa 22 zilizopita Waziri huyo alitoa zawadi ya shilingi milioni 50 na akafuatisha ujumbe unaosema idadi kubwa ya watu walijitokeza wakitaka kufanya shughuli ambayo hakubainisha ilikuwa kuwatunuku kwa sababu gani.

"Idadi kubwa ya watu wamejitokeza kufanya shughuli hiyo ata kwa shilingi milioni 10 pekee si ata shilingi milioni 50 nilizokuwa nikitoa hapo awali. Mnataka niwatunuku aje?” Moses Kuria aliwauliza wafuasi wake mitandaoni.

Jumbe hizi hazikupolewa vyema huku wengi walieleza kuwa zilikiuka tabia anazopaswa kuwa nazo kiongozi wa haiba ya juu kama waziri.