Martha Karua: Eneo la mlima Kenya halitatumika kama mbadala tukitazama

Kulingana naye eneo la mlima Kenya halitatumika kama mbadala na serikali ya Rais William Ruto.

Muhtasari
  • Akihutubia wanahabari siku ya Jumanne, Karua alisema Raila yuko katika mazungumzo mengine muhimu na hangeweza kuungana nao.
JEREMIAH KIONI,MARTHA KARUA NA PETER MUNYA
Image: TWITTER

Kiongozi wa chama cha NARC Kenya Mhe Martha Karua amejibu kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter dakika chache baada ya mkutano wake wa kiamsha kinywa na waziri wa zamani wa Uhuru Kenyatta Peter Munya, na  katibu mkuu wa zanani waJubilee Mhe Jeremiah Kioni.

Kulingana naye eneo la mlima Kenya halitatumika kama mbadala na serikali ya Rais William Ruto.

Alitumia ukurasa wake rasmi wa twitter kushiriki picha zake, Jeremiah Kioni na Peter Munya.

"Mkutano wa kifungua kinywa na viongozi wa kamwene. Kanda ya Mlima Kenya halitatumika kama mbadala kama tunavyotazama". Alisema Mhe. Martha Karua kiongozi wa chama cha NARC Kenya.

Kesho Martha Karua, Jeremiah Kioni na Peter Munya huenda wakashikilia Maandamano katika eneo la Mlima Kenya dhidi ya serikali ya rais William Ruto.

Kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua ameeleza ni kwa nini kiongozi wa Azimio Raila Odinga hakuwepo wakati wa  waandishi wa habari wa Azimio siku ya Jumanne.

Akihutubia wanahabari siku ya Jumanne, Karua alisema Raila yuko katika mazungumzo mengine muhimu na hangeweza kuungana nao.

"Samahani kwamba kiongozi wetu Raila Odinga hayuko nasi. Yuko katika mazungumzo mengine muhimu na tulizungumza naye na tutamripoti maendeleo kufikia sasa," alisema.

Hata hivyo, Karua alishikilia kuwa maandamano yaliyopangwa kufanyika Jumatano, Alhamisi na Ijumaa yanaendelea.

Raila aliitisha maandamano ya siku tatu mitaani kama sehemu ya kushinikiza utawala wa Rais William Ruto.

Alikataa wito wa kusimamisha maandamano akisema Wakenya wana haki chini ya Katiba ya 2010 kufanya maandamano dhidi ya mamlaka.

Siku ya Jumanne, takriban mabalozi 13 wa Ulaya walitoa wito kwa Ruto na Raila kukumbatia mazungumzo ili kukomesha hasara zaidi ya maisha.

Katika taarifa yao ya pamoja, mabalozi na Makamishna Wakuu walisema wanasikitishwa na vurugu na kupoteza maisha.