Uchumi wa Kenya katika hali mahututi kwa sababu ya sera mbovu, sio maandamano - Raila

“Unalaumu utawala wa Rais wa Awali Uhuru Kenyatta kwa hali ya uchumi nchini ilhali aliondoka serikalini mwaka jana Septemba,” alisema Raila.

Muhtasari

• Raila Odinga amesema uchumi uko katika hali mbaya si kwa sababu ya maandamano yaliyoandaliwa na muungano huo bali sera mbovu za serikali.

Kinara wa upinzani Raila Odinga
Kinara wa upinzani Raila Odinga
Image: MAKTABA

Kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga amesema uchumi uko katika hali mbaya si kwa sababu ya maandamano yaliyoandaliwa na muungano huo bali sera mbovu za serikali.

Akihutubia vyombo vya habari vya kimataifa Jumanne, Raila alisema kuwa serikali imekuwa ikimlaumu Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ilhali wamekopa zaidi ya alivyokopa.

“Unalaumu utawala wa Rais wa Awali Uhuru Kenyatta kwa hali ya uchumi  nchini ilhali aliondoka serikalini mwaka jana Septemba,” akasema.

Kiongozi huyo wa chama cha ODM, aliongeza kuwa serikali hii imehudumu kwa muda wa miezi 10 tayari na bado lalama zao ni kuwa Rais mstaafu Kenyatta alikuwa akikandamiza hatua zao za kujaribu kufufua Uchumi.

"Sasa tuko Julai na mmeendesha serikali hii kwa miezi 10 iliyopita. Tulitarajia kuona mabadiliko fulani ndani ya muda huo."

Wakati wa kuapishwa baada ya kuibuka akama washinda wa uchguzi wa mwaka 2022, Naibu Rais Gachagua alibainisha kuwa walikuwa walirithi serikali iliyodorora kutoka kwa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Alibainisha kuwa kuna changamoto ya upatikanaji wa fedha za maendeleo kwa sababu kiasi kinachokusanywa na Hazina ya Taifa kinatumika kulipa mishahara na kulipa madeni.

"Nataka kurudia ili tena. Tumerithi uchumi uliodorora na tuna kazi ya kufanya kugeuza uchumi wa nchi hii na tutakuwa na wito kwenu nyote mtuvumilie kwa sababu si  kazi rahisi," Gachagua alisema.

Raila amekuwa kimya na hakujitokeza wakati wa maandamano akidai kuwa alikuwa akiugua homa na hakuweza kujitokeza na kujinga na wafuasi wake waliolekea mitaani kuandamana kwa sababu ya gharama ya juu ya hali ya maisha.