Ruto awafunza wajumbe salamu za kiswahili katika kongamano la Tabianchi

Ruto alichukua hatua hiyo katika siku ya pili ya mkutano huo unaotarajiwa kuendelea hadi Jumatano.

Muhtasari
  • Aliwataka viongozi hao kujisikia wako nyumbani na kutenga muda wa kutembelea vituko vya nchi.
  • Ruto alizindua rasmi mkutano huo siku ya Jumatatu ambao unaandaliwa pamoja na Kenya na Muungano wa Afrika.
  • Ruto aliwakaribisha wajumbe wote walioitikia wito wa kuhudhuria mkutano huo.
Image: ENOS TECHE

Rais William Ruto mnamo Jumanne aliwafunza viongozi na wajumbe katika Mkutano wa Hali ya Hewa wa Afrika salamu za Kiswahili ili kuwasaidia katika maingiliano yao na Wakenya.

Ruto alichukua hatua hiyo katika siku ya pili ya mkutano huo unaotarajiwa kuendelea hadi Jumatano.

"Hizi ni salamu ili tu utafute njia. 'Jambo' ndiyo salamu. Mtu akikwambia 'jambo' unamjibu kwa 'jambo' ni rahisi," alisema Jumanne.

Rais alitangulia kuusalimia umati kwa kusema 'jambo' na akapata majibu.

Kisha Ruto akawafundisha viongozi na wajumbe jinsi ya kusema 'habari zenu' kwa Kiswahili.

“Unapotaka kusema ‘habari yako’ unasema ‘mambo’ Rahisi, halafu jibu ni ‘poa’’, alisema huku akiendelea kuusalimia umati huo alipokuwa ametoka kuwafundisha.

"Kwa hivyo nina hakika utapata njia yako na salamu hizo," Rais alisema.

Aliwataka viongozi hao kujisikia wako nyumbani na kutenga muda wa kutembelea vituko vya nchi.

Ruto alizindua rasmi mkutano huo siku ya Jumatatu ambao unaandaliwa pamoja na Kenya na Muungano wa Afrika.

Ruto aliwakaribisha wajumbe wote walioitikia wito wa kuhudhuria mkutano huo.

Ninawakaribisha wote kwenye Mkutano wa Hali ya Hewa wa Afrika. Hujaingia tu katika ukumbi wa mikutano bali katika siku zijazo. Huu sio mkutano wa kawaida, "alisema.

Alisema mkutano huo ambao umepangwa kuanzia Septemba 4 hadi 6 unalenga kuelezea Afrika kama sehemu ya suluhisho la mgogoro wa hali ya hewa.

Ruto alisema sio mkutano wa kilele wa michezo ya lawama bali ni mkutano ambapo kila mtu huja mezani kutafuta suluhu.

"Sote tumekutana hapa kwa ajili ya mkutano wa kwanza kabisa wa hali ya hewa barani Afrika ili kuja na suluhu katika kukabiliana na mzozo wa hali ya hewa," alisema.