Willis Raburu ajiuzulu kama mwenyekiti wa kamati ya tamasha la Nairobi

Alisema ili Nairobi iwe na maendeleo katika sekta mbali mbali, uamuzi kama huo unahitajika ili kuleta mabadiliko.

Muhtasari

•Katika taarifa yake ya Oktoba 30, Raburu alitangaza wazi kuwa amejiuzulu kutoka kwa kamati hiyo ya tamasha la kaunti ya Nairobi.

•Raburu alidai kuwa ni wakati mwema wa kuwapa watu wengine nafasi ya kutoa uongozi na huduma bora kwa watu.

Wilis Raburu/Instagram
Wilis Raburu/Instagram

Mwanahabari Willis Raburu ambaye alikuwa mwenyekiti  wa kamati ya kuandaa tamasha la kaunti ya Nairobi,ametangaza  rasmi kujiuzulu kutoka wadhfa huo.

Katika taarifa yake mnamo Oktoba 30, Raburu alitangaza wazi kuwa amejiuzulu kutoka kwa kamati hiyo.

“Asubuhi ya leo, nimeujuza rasmi uongozi wa kaunti kwamba sitahudumu katika nafasi yangu ya sasa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Nairobi,” ilisoma taarifa hiyo kwa sehemu.

Alichukua fursa hiyo kumshukuru gavana Sakaja, akisema kuwa ni heshima kubwa  yeye kumpa jukumu hilo na kushukuru kwa uaminifu waliokuwa nao kwake wakati wa huduma zake.

“Imekuwa heshima kufanya kazi pamoja na Gavana Sakaja na utawala wake, na mimi ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa uaminifu na fursa waliyonayo kwangu kwa muda huo.”

Akitoa sababu zake za kujiuzulu,amedai kuwa ni wakati mwema wa kuwapa watu wengine nafasi ya kutoa uongozi na huduma bora kwa watu.

“Walakini, uamuzi huu umeafikiwa na utambuzi wa hitaji kubwa la kimfumo na mabadiliko ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma na uongozi, ili kuhudumia vyema kaunti na wakazi wake, mtazamo wa kina zaidi unahitajika ambao tayari umwkweisha anzishwa na nawatakia kila la heri katika suala hili,”alieleza.

Aidha alisema kuwa ili Kaunti ya Nairobi kuwa na maendeleo katika sekta mbali mbali,uamuzi kama huo unahitajika ili kuleta mabadiliko.

“Ninaamini  kwamba ili kuwa na mabadiliko chanya, tunaweza kutengeneza njia kwa mustakabali mwema. Tumaini langu ni kwamba uamuzi huu utatumika kama kielelezo cha mabadiliko muhimu ambayo kaunti yetu inaitaji.

Raburu alichukua uongozi kama mwenyekiti wa kamati ya tamasha la Nairobi siku chache baada ya kujiuzulu kama mtangazaji wa Runinga ya Citizen baada ya kuhudumu kwa kipindi cha zaidi ya muongo mmoja.