Zifahamu kaunti 10 zitakazoathirika na kukatizwa kwa umeme Alhamisi- KPLC

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa Alhamisi, Desemba 14.

Muhtasari

•KPLC itangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti kumi za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Machakos, Kajiado,Uasin Gishu, Nyeri, Embu, Nandi, Kisii, Kiambu, Migori na Kilifi. 

Kenya Power

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Desemba 14.

Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti kumi za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Machakos, Kajiado,Uasin Gishu, Nyeri, Embu, Nandi, Kisii, Kiambu, Migori na Kilifi. 

Katika kaunti ya Machakos, mji wa Mlolongo na sehemu za maeneo ya Sabaki, Ilpolosat na Konza yataathirika na kukatizwa kwa umeme kulikopangwa kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za eneo la Kiserian katika kaunti ya Kajiado zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Uasin Gishu, sehemu za maeneo ya Cheplaskei na Kabiyet zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu nyingi za kaunti ya Nyeri pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Miongoni mwa maeneo ya Nyeri ambayo yataathirika ni pamoja na Tetu, Kigogoini, Wandumbi, Chaka, Karundas, Chinga na Ruruguti.

Katika kaunti ya Embu, eneo la PI Oriental Hotel litakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu za maeneo ya Koisolik na Kurgung katika kaunti ya Nandi pia zitakosa umeme kati ya saa nne asubuhi na saa moja jioni.

Katika kaunti ya Kisii, maeneo ambayo yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri ni pamoja na Ogembo na Kenyenya. Wakati huohuo, maeneo ya Kegonga na Maeta katika kaunti ya Migori pia yataathirika.

Katika kaunti ya Kiambu, sehemu za maeneo ya BTL, Prisons, Superfoam, MKU, Bidco, Witeithie na Bob Harries Road pia yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za mji wa Kilifi katika eneo la Pwani pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.