Sonko ajitenga na programu ya mkopo wa simu inayowalaghai Wakenya kwa picha yake

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, Sonko alidai kwamba hakuwa na uhusiano wowote na programu hiyo.

Muhtasari
  • Kampuni ya kifedha inayoendesha akaunti kwa jina ‘Mike Sonko Rescue Loans’ ilichapisha tangazo lililofadhiliwa kwenye mtandao wa kijamii ikidai kuwa kwa ushirikiano na Mike Sonko.
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Image: Facebook//Mike Sonko

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko amejitenga na programu ya kidijitali inayodai kushirikiana naye katika kutoa mikopo kwa Wakenya.

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, Sonko alidai kwamba hakuwa na uhusiano wowote na programu hiyo.

"Kuna programu hii inazunguka kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa wanashirikiana na mimi kutoa mikopo kwa umma. Natamani kujitenga nayo,” alisema kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

"Inaendeshwa na walaghai ambao wanajaribu kula pesa kutoka kwa wanachama wa umma," aliongeza, akionya umma kuhusu wizi wa utambulisho.

Kampuni ya kifedha inayoendesha akaunti kwa jina ‘Mike Sonko Rescue Loans’ ilichapisha tangazo lililofadhiliwa kwenye mtandao wa kijamii ikidai kuwa kwa ushirikiano na Mike Sonko.

Chapisho hilo lilionyesha zaidi kwamba kampuni hiyo ilishirikiana na programu ya huduma ya msaada wa kifedha ya Mkopo Extra ili kuwapa Wakenya maskini hadi Ksh100,000.

Mkopo Extra, kwa Ubia na Mike Sonko, inatoa msaada wa mkopo kwa Wakenya wote. Pokea hadi Ksh 100,000 papo hapo,” chapisho hilo ambalo Sonko alidai lilikuwa ghushi.

Akaunti ya ‘kampuni ya kifedha’ ina zaidi ya wafuasi 2.5k kwenye Facebook, na picha ya Sonko akiwa ameshikilia bunda la pesa kama picha yake ya wasifu na picha ya jalada.