Raila aifariji familia ya mwenyekiti wa ODM Migori Makabong'o

“Alitoa wito kwa uongozi wa chama cha kaunti kusimama pamoja na kusaidia familia wakati wanajiandaa kumzika Bw Makabong’o

Muhtasari
  • Katika taarifa ya chama cha Orange Party, Raila aliihakikishia familia ya Makabong'o uungwaji mkono wake haswa katika wakati mgumu unaowakabili.
Raila Odinga
Raila Odinga
Image: Facebook

Kinara wa ODM Raila Odinga ametuma risala za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu Philip Makabong'o ambaye alikuwa mwenyekiti wa ODM Kaunti ya Migori.

Katika taarifa ya chama cha Orange Party, Raila aliihakikishia familia ya Makabong'o uungwaji mkono wake haswa katika wakati mgumu unaowakabili.

“Alitoa wito kwa uongozi wa chama cha kaunti kusimama pamoja na kusaidia familia wakati wanajiandaa kumzika Bw Makabong’o,” taarifa hiyo inaongeza.

Chama kilikubali kujitolea, ujasiri na azimio la mtu huyo katika utumishi wake, na kuongeza kuwa hakuwahi kuyumba hata katika nyakati ngumu.

Kwa mara ya kwanza chama kilitangaza kuaga kwa Makabong'o, siku ya Jumapili.