Miguna amgeuzia Ruto mtutu wa mahsambulizi baada ya kuishambulia idara ya mahakama

“Hivi ndivyo udikteta unavyoanza. Inaingia wakati nchi ina njaa, imechoka na kukata tamaa" Miguna alisema.

Muhtasari

• “Hatuwezi kuruhusu mtu yeyote aigeuze mahakama kuwa taasisi yenye woga, vitisho na majungu kwa sababu hilo haliwezi kuwa na maslahi kwa wananchi." alisema.

MIGUNA MIGUNA AOMBA RAIS KUONDOA KESI YAKE KAMA ALIVYOAHIDI
MIGUNA MIGUNA AOMBA RAIS KUONDOA KESI YAKE KAMA ALIVYOAHIDI

Wakili Miguna Miguna ambaye kwa muda sasa amekuwa akitetea sera za rais William Ruto ameonekana kubadili msimamo pindi tu baada ya kiongozi huyo wa taifa kuishambulia idara ya mahakama akidai kwamba kuna ufisadi unaoendelewa mle.

Miguna alianzisha muendelezo wa kashfa dhidi ya Ruto kupitia ukurasa wake wa Xakidai kwamba kwa kuanza kuishambulia idara huru ya mahakama, udikteta unaanza kwa njia hiyo.

“Hivi ndivyo udikteta unavyoanza. Inaingia wakati nchi ina njaa, imechoka na kukata tamaa. Huanza kwa kuua taasisi na maeneo yaliyopangwa ambayo yangewalinda watu dhidi ya ulafi unaofanywa na walio madarakani.”

“Hatuwezi kuruhusu mtu yeyote aigeuze mahakama kuwa taasisi yenye woga, vitisho na majungu kwa sababu hilo haliwezi kuwa na maslahi kwa wananchi. Tunahitaji mahakama imara, INAYOJITEGEMEA, yenye uwezo na AKILI. Hatuwezi kujenga moja kupitia vitisho vya watendaji, vitisho, shuruti, au hongo!” Miguna alisema.

Aidha, wakili huyo ambaye aliwezehwa kurudi nchini baada ya miaka 4 uhamishoni kayika utawala uliopita alimkashfu vikali mchambuzi wa masuala ya kisiasa Mutahi Ngunyi kwa kumshauri Ruto kupuuza sheria na maagizo ya mahakama ili kuendeleza ajenda zake.

“Bwana @MutahiNgunyi: Huna sifa ya kumshauri yeyote kuhusu ufisadi. Umeoza hadi mwisho. Uliiba pesa za umma kupitia kashfa ya NYS lakini hujaadhibiwa kwa hilo. Ulichoma nyumba yako kwa makusudi miaka michache iliyopita na kuiba pesa za bima,” alimwambia.

Mjadala mkali umeibuka katika siku za hivi karibuni baada ya rais Ruto kudokeza hadharani kwamba hatosikiliza wala kuheshimu agizo lolote la mahakama linalolenga kusitisha ajenda zake za maendeleo kwa Wakenya.

Ruto akizungumza katika hafla ya mazishi ya babake seneta wa Nyandarua, John Methu, alisema kwamba ni wakati sasa umefika wawe na mahojiano na idara ya mahakama, akidai kwamba kuna watu wanahonga majaji ili kubatilisha sheria ambazo zinapitishwa na bunge kwa ajili ya maendeleo kwa wananchi.