KCSE2023: Watahiniwa 48,174 wapata alama ya E, asilimia kubwa ikiwa ni wavulana

“Nimeumizwa na ukweli kwamba idadi kubwa ya watahiniwa (48,174 au 5.33%) bado waliishia kupata alama ya wastani ya E katika Mtihani wa KCSE wa 2023" Waziri alisema.

Muhtasari

• Waziri pia alisema kuna Zaidi ya wanafunzi elfu 4 ambao walipatinana wakijihusisha katika visa vya udanganyifu katika mitihani na watajua hatima yao baadae.

CS Machogu.
CS Machogu.
Image: X

Kila mwaka wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne KCSE, asilimia ya wale wanaopata alama za chini kabisa aghalabu huwashangaza wengi.

Katika matokeo ya mwaka 2023 ambayo yalitangazwa mapema asubuhi ya Jumatatu Januari 8 na waziri wa elimu Ezekiel Machogu kutoka shule ya upili ya wasichana na Moi mjini Eldoret, watahiniwa 48,174 kati ya 889,453 idadi jumla ya wanafunzi walioketi mitihani hiyo walipata alama ya E, ikiwa ni asilimia 5.33 ya idadi jula.

Kati ya hao, asilimia kubwa ilikuwa watoto wa kiume, wakiwa 28,214, na wasichana wakiwa 19, 960.

“Nimeumizwa na ukweli kwamba idadi kubwa ya watahiniwa (48,174 au 5.33%) bado waliishia kupata alama ya wastani ya E katika Mtihani wa KCSE wa 2023 hata baada ya Wizara kutumia mfumo unaonyumbulika zaidi wa kukokotoa matokeo ya mwisho ya watahiniwa wa jumla.”

Waziri pia alisema kuna Zaidi ya wanafunzi elfu 4 ambao walipatinana wakijihusisha katika visa vya udanganyifu katika mitihani na watajua hatima yao baadae.

“Matokeo ya watahiniwa 4,109 waliosalia ambao walishukiwa kujihusisha na makosa ya mitihani yamezuiliwa kusubiri upelelezi wa kesi zao kukamilika,” alsiema.