Kwa nini matokeo ya KCSE 2023 hayatapatikana kwa njia ya SMS

Huduma ya kuoata matokeo ya mitihani ya kitaifa ya KCPE mwaka jana ilitatizika na watu wengi walilalamika kutopokea matokeo licha ya kutuma ujumbe mfupi na hata kukatwa vocha yao ya shilingi 25.

Muhtasari

• "Utahitajika kuweka nambari ya faharasa ya mtahiniwa wako na jina/majina kulingana na data ya usajili wa mtihani wa KCSE wa 2023,” Machogu alisema.

Waziri wa Elimu,Ezekiel Machogu
Waziri wa Elimu,Ezekiel Machogu
Image: MAKTABA

Kwa mara ya kwanza katika muda mrefu, matokeo ya mtihani wa kitaifa wa KCSE 2023 hayatapatikana kupitia njia ya ujumbe mfupi.

Akitangaza matokeo hayo kutoka shule ya upili ya wasichana ya Moi mjini Eldoret, waziri Machogu alisema kwamba safari hii kwa bahati mbaya watahiniwa hawatoweza kufikia matokeo yao kwa Kutuma namba zao za index kwa ujumbe mfupi wa SMS ambao aghalabu kuhitaji mtu kuwa na angalau vocha ya shilingi 25 ili kufanikisha mchakato huo.

“Mtahiniwa anaweza kufikia matokeo binafsi ya KCSE 2023 mtandaoni kupitia kiungo kwenye tovuti ya KNEC au moja kwa moja kupitia URL: https://results.knec.ac.ke. Utahitajika kuweka nambari ya faharasa ya mtahiniwa wako na jina/majina kulingana na data ya usajili wa mtihani wa KCSE wa 2023,” Machogu alisema.

Hati rasmi za matokeo zitapatikana kupitia vituo vya mitihani ambapo watahiniwa walifanyia mitihani yao.

Huduma ya kuoata matokeo ya mitihani ya kitaifa ya KCPE mwaka jana ilitatizika na watu wengi walilalamika kutopokea matokeo licha ya kutuma ujumbe mfupi na hata kukatwa vocha yao ya shilingi 25.

Kufuatia mkanganyiko huo ambao ulichukua Zaidi ya saa mbili kutatuliwa, waziri machogu alitangaza kuwa Wizara ya Elimu ilikuwa inachunguza kusitisha matumizi ya huduma ya SMS kukagua matokeo ya mitihani ya kitaifa.