Tazama maeneo ambayo hayatakuwa na stima leo, Jumapili

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni

•Sehemu za maeneo ya Ngong-Kibiko-Kimuka-Saikeri katika kaunti ya Kajiado pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. 

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili.

Katika taarifa ya Jumamosi jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi,Machakos, Kajiado na Nyeri.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za eneo la Karen itaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Miongoni mwa sehemu zitakazoathirika ni pamoja na Dagoretti Rd, Warai, Kituo cha polisi cha Karen, Ololua Close, Kerarapon Rd, Windy Ridge pamoja na zingine.

Sehemu za maeneo ya Ngong-Kibiko-Kimuka-Saikeri katika kaunti ya Kajiado pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Mji wa Kajaido, Kibiko, Suswa Rd ni miongoni mwa sehemu zitakazoathirika.

Katika kaunti ya Machakos, sehemu ya barabara kuu ya Mombasa zikiwemo Brava Foods, Swara Acacia Lodge, Kusyombuguo na, Game Ranch zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Baadhi ya sehemu kando ya barabara ya Konza/Mombasa pia zitaathirika.

Sehemu za mji wa Nyeri na Witemere katika kaunti ya Nyeri pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Baadhi ya sehemu zitakazoathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Blue Valley, Kungu Maitu, Afisi ya gavana na viunga vyake.