Tazama maeneo ambako hakutakuwa na stima leo, Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Katika kaunti ya Kisii, sehemu za maeneo ya Kegogi na Manga Isecha yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Kenya Power

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne.

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kakamega, Kisii na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kahawa Sukari na Kilimani zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Kaburengu na Butali Sugar katika kaunti ya Kakamega pia yataathirika na kukatizwa kwa umeme siku ya Jumanne kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na nusu alasiri.

Katika kaunti ya Kisii, sehemu za maeneo ya Kegogi na Manga Isecha yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya mji wa Kilifi, Mtondia na Tezo katika kaunti ya Kilifi pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme siku ya Jumanne kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi alasiri.