Maeneo ya Kenya yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme Jumatano

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kajiado, Machakos na Embu.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano.

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba maeneo kadhaa katika kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kajiado, Machakos na Embu.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya barabara ya Langata na Bomas zikiwemo Karen Hospital, Mukinduri Estate, Amara Ridge, Mokoiyet na kwingineko zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za eneo la Nkoroi katika kaunti ya Kajiado zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Miongoni mwa sehemu zitakazoathirika ni pamoja na Barabara mpya, Mayor Road, Rangau Citam na viunga vyake.

Katika kaunti ya Machakos, sehemu za barabara ya Mombasa zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Muthama Heights, Hilton Garden Inn, Banbros, Steel Wool Africa na Signode ni baadhi tu ya sehemu zitakazoathirika.

Sehemu za maeneo ya Mutunduri, Kirigi, Mungania T/Factory na Kianjokoma katika kaunti ya Embu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa nane mchana.