Safaricom yafafanua sababu ya baadhi ya wateja kutopokea meseji za M-Pesa

Safaricom walibaini kwamba malalamiko mengi yalikuwa yakitoka kwa wateja watumizi wa smartphones za Android.

Muhtasari

• Kwa msisitizo, Safaricom iliwataka wateja wote wanaotumia simu za Android kutumia programu stahiki za SMS kwa vile hiyo program huwa haifichi jumbe.

CEO PETER NDEGWA
Image: MAKTABA

Kampuni ya mawasiliano nchini Safaricom imesikitishwa na taarifa zilizowafikia kutoka kwa baadhi ya wateja kwamba kwa muda sasa hawajapokea ujumbe wowote kutoka Safaricom au M-Pesa pindi wanapofanya miamala.

Kupitia kurasa zao rasmi kwenye mitandao ya kijamii, Safaricom walisema kwamba sehemu ya wateja wake aghalabu watumizi wa simu za smartphones ndio walioathirika na hilo kwani hawapokei ujumbe wowote kutoka Safaricom.

Ili kutatua hilo, Safaricom ilibaini kwamba huenda wale wanaokosa kuona meseji pengine wantumia program za kuleta meseji ambazo si zile zilizokuja na simu yenyewe.

Ili kutoa utatuzi huo, Safaricom iliorodhesha njia tatu muhimu za wateja kufuata ili kurejesha hali ya kawaida katika simu zao ili kuwawezesha kuona jumbe za M-Pesa kwenye simu zao.

“Kwanza fungua program ya SMS ya simu yako na uangalie kwenye kitufe cha Spam & Blocked, kisha uangalia kama kuna ujumbe wowote wa Safaricom au M-Pesa na ufanye unblock. Meseji nyingine zifuatazo zitakuwa zinaingia kwenye Inbox stahiki ya jumbe zako zote,” Safaricom ilitoa maelezo.

Kwa msisitizo, Safaricom iliwataka wateja wote wanaotumia simu za Android kutumia programu stahiki za SMS kwa vile hiyo program huwa haifichi jumbe.