Sehemu kadhaa za kaunti 5 kukosa umeme Siku ya Wapendanao - KPLC

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Februari 14.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Februari 14.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Machakos, Makueni, Kajiado, Nandi, Kisii.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Athi River na Kaumoni katika kaunti ya Machakos zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Makueni, baadhi ya sehemu za eneo la Kibwezi zitakosa umeme katio ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, baadhi ya sehemu za eneo la Lower Matasia katika kaunti ya Kajiado pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kamagut na NTSA katika kaunti ya Nandi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Kisii, baadhi ya sehemu za maeneo ya Kiamokama na Ibacho zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa unusu alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Mwembe na Kiamabundu katika kaunti hiyo pia zitakosa umeme kati ya saa nne unusu asubuhi na saa nane mchana.