KPLC yatangaza maeneo ambayo yatakuwa bila stima Alhamisi

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Februari 15.

Muhtasari

•KPLC imetangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Homa Bay, Embu, Meru, Kiambu, Kitui na Mombasa.

Kenya Power

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Februari 15.

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Homa Bay, Embu, Meru, Kiambu, Kitui na Mombasa.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za maeneo ya Rosslyn, Kitsuru, Gate Industrial Park, Karen na Joska zitaathirika na kukatizwa na umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Pala, Ngeta na Sombro katika kaunti ya Homa Bay zitakuwa bila stima kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa tisa unusu alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kimangaru na Itabua Secondary katika kaunti ya Embu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Meru, sehemu mbalimbali za maeneo ya Gitoro, Kiirua na Ntugi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, baadhi ya sehemu za maeneo ya mji wa Juja na hospitali ya Kalimoni pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Mbondoni na Nguutani katika kaunti ya Kitui zitakuwa bila stima kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Mikindani katika kaunti ya Mombasa zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.