KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa stima leo, Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Machi 19.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Uasin Gishu, Nyeri, Kirinyaga, Homa Bay na Kilifi.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Machi 19.

Katika taarifa ya siku ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Uasin Gishu, Nyeri, Kirinyaga, Homa Bay na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, maeneo ya Chuo Kikuu cha Kenyatta, Lavington na Westlands yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Kiukenda na Kiamumbi katika kaunti ya Kiambu zitaathirika na kukatizwa kwa stima kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Chaka, Karundas, Mbiriri Gitugi Tea Factory katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Uasin Gishu, sehemu kadhaa za maeneo ya Leseru na Lower Sosian zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Kirinyaga, sehemu za maeneo ya Kagumo na Mutira zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Gendia na Simbiri katika kaunti ya Homa Bay zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Sehemu kadhaa za eneo la Vipingo katika kaunti ya Kilifi pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.