KPLC yatangaza maeneo ambayo kutakuwa na kukatizwa kwa umeme leo, Jumamosi

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumamosi, Machi 23. .

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Sehemu kadhaa za maeneo ya Kipsingori na Karara katika kaunti ya Trans Nzoia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumamosi, Machi 23. .

Katika taarifa ya siku ya Ijumaa jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Trans Nzoia, Bungoma, Lamu na Tana River.

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za eneo la Joska  Feeder zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kipsingori na Karara katika kaunti ya Trans Nzoia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Nabuyole Falls na mji wa Webuye zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane alasiri. Eneo la Hospitali ya Bungoma pia litaathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Lamu, eneo la kisiwa cha lamu na viunga vyake litakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Hola na Masalani katika kaunti ya Tana River pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.