Tazama maeneo ambayo yataathirika na kukatizwa kwa stima Jumatano -KPLC

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Tharaka Nithi, Kiambu na Kilifi.

Muhtasari

•KPLC imetangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti nne yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano. Machi 27.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Tharaka Nithi, Kiambu na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za barabara ya Waiyaki na ya Raphta zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Kianjagi na afisi za kaunti za Chogoria katika kaunti ya Tharaka Nithi zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Toll Station na Murera Coffee katika kaunti ya Kiambu yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za eneo la Watamu katika kaunti ya Kilifi zitaathirika na kukatizwa na umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.