KPLC yatangaza maeneo yatakayokosa stima leo, Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Aprili 2.

Muhtasari

•KPLC imetangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Makueni,Bomet, Homa Bay, na Nyeri.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Aprili 2.

Katika taarifa ya siku ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Makueni,Bomet, Homa Bay, na Nyeri.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za maeneo ya Muthaigana Nairobi West zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, baadhi ya sehemu za eneo la Kaumoni katika kaunti ya Makueni pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.

Sehemu kadhaa za eneo la Tenwek katika kaunti ya Bomet pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi jioni.

Katika kaunti ya Homa Bay, baadhi ya sehemu za maeneo ya Rusinga na Kaswanga zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Giakanja katika kaunti ya Nyeri pia litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.