Tumepoteza watu 1,213 kwenye ajali za barabarani katika kipindi cha miezi 3 - CS Murkomen

“Wenye wamekufa Zaidi ni watu wako huko mashinani, mijini. Unaona mpaka sasa tumepoteza watu 283 waliokuwa wakiendesha pikipiki, na weney walikuwa wamebeba kwa hiyo pikipiki, tumepoteza watu 103,” alisema.

Muhtasari

• Waziri huyo alisema mwaka jana, kipindi sawia na hicho, Kenya ilikuwa imepoteza 1,146, ikiwa chini kwa watu 67 ambao wamefariki kipindi kama hicho mwaka huu.

KIPCHUMBA MURKOMEN
KIPCHUMBA MURKOMEN
Image: x

Waziri wa barabara na miundombinu mingine Kipchuma Murkomen hatimaye amezungumzia kuhusu kero la ajali za barabarani ambazo zimeonezeka katika kipindi cha wiki za hivi karibuni.

Murkomen ambaye alijiunga na viongozi wengine katika kituo cha mafunzo ya kidini kanisa la AIC Narok, Murkomen alisema wizara yake haifai kulaumiwa kutokana na ongezeko hilo na kusema ni jukumu la kila Mkenya kuwajibikia usalama barabarani.

Waziri huyo pia alikwenda mbele na kutoa takwimu za jinsi ajali zimekuwa zikigharimu idadi tofauti ya maisha katika miaka ya nyuma ikiwemo idadi ya waliokufa kutokana na ajali katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

“Wakati sisi tuliingia ofisini mwaka jana, tulikuwa tumepoteza watu 4,650 mwaka 2022, mwaka jana tulipunguza kidogo ikakuja 4,300. Mwezi huu tunavyoongea sasa hivi, tayari takwimu ambazo nimetumiwa, tayari tumepoteza watu 1,213 katika miezi 3! Watu wenye afya nzuri tu walikuwa wanasafiri,” Murkomen alisema kwa masikitiko.

Waziri huyo alisema mwaka jana, kipindi sawia na hicho, Kenya ilikuwa imepoteza 1,146, ikiwa chini kwa watu 67 ambao wamefariki kipindi kama hicho mwaka huu.

Murkomen alisema kwamba vifo vingi vimetokana na kuendesha pikipiki huku abiria wa pikipiki hizo pia wakiwa waathirika wengi.

“Wenye wamekufa Zaidi ni watu wako huko mashinani, mijini. Unaona mpaka sasa tumepoteza watu 283 waliokuwa wakiendesha pikipiki, na weney walikuwa wamebeba kwa hiyo pikipiki, tumepoteza watu 103,” alisema.

Aidha, waziri huyo alisema kufikia sasa wale ambao wamepotea katika ajali za magari ni 271 na wale wamegongwa na magari wakivuka barabara ni watu 445.