Kizaazaa Mchina akirejea na kupata nyumba yake iliuzwa wakidhani alikufa kwa Corona (video)

Mzee huyo raia wa Uchina alisema aliondoka nchini 2016 kwenda kwao kwa na kabla hajarudi, janga la Covi-19 likabisha na baadae watu wakadhani alikufa kwa janga hilo kisha kupiga mnada nyumba yake kwa milioni 80.

Muhtasari

• Pia alieleza sababu nyingine iliyomzuia kurudi mapema ni pasipoti yake ya kusafiria kuisha muda wa matumizi, hivyo akalazimika kuanza upya mchakato wa kupata nyingine.

Mchina arudi na kupata nyumba imeuzwa
Mchina arudi na kupata nyumba imeuzwa
Image: Screegrab// Wasafi Media (YouTube)

Kizaazaa kilishuhudiwa katika mji wa Mbeya jijini Tanzania baada ya mzee raia wa Uchina kurejea na kupata nyumba yake iliuzwa kitambo kwa kile alitaja kuwa walidhani alikufa kutokana na janga la Corona mapema 2020.

Kwa mujibu wa taarifa, nyumba yake iliuzwa na watu kwa shilingi milioni 80 za kitanzania, baada ya mzee huyo kwenda kwao Uchina na kukawia kurudi.

Mzee huyo alieleza aliondoka Tanzania mwaka 2016 kwa ajili ya shughuli za kifamilia lakini kabla hajarejea, janga la Covid-19 likabisha.

Hapo ndipo alilazimika kuongeza kipindi cha kukaa kwao Uchina kwani kusafiri kulipigwa marufuku kama njia moja ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Pia alieleza sababu nyingine iliyomzuia kurudi mapema ni pasipoti yake ya kusafiria kuisha muda wa matumizi, hivyo akalazimika kuanza upya mchakato wa kupata nyingine.

Baada ya kufanikisha michakato yote na kurejea Aprili 2024, alipigwa na butwaa kupata nyumba yake iko chini ya umiliki mpya, akiambiwa kwamba iliuzwa wakidhani aliangamia kwa Corona.

“Mimi 2016 nilienda China, huko Corona ikafunga, hamna kusafiri, baadae ikafunguliwa na nikapata pasipoti nyingine nikaja, kufika huku nikapata tayari nyumba yote imeuzwa, wakisema nilienda China nikafa kwa Corona, wakasema haraka uza nyumba,” Mchina huyo alibananga kiswahili.

Tazama video ya kisa hicho cha kushangaza hapa;