Maeneo yatakayokabiliwa na kukatizwa kwa umeme leo, Jumapili- KPLC

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Aprili 21.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Baadhi ya sehemu za maeneo ya Parklands na Pangani zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Aprili 21.

Katika taarifa ya siku ya Jumamosi jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Bungoma, Kisumu, Kisii, Kilifi, Lamu, na Tana River.

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za maeneo ya Parklands na Pangani zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za eneo la Nambale DC katika kaunti ya Bungoma zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa nane mchana.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Katolo na Nyakongo katika kaunti ya Kisumu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Kisii, sehemu kadhaa za mji wa Kisii zitakumbwa na matatizo ya umeme kati ya saa moja unusu asubuhi na saa nane unusu mchana.

Baadhi ya sehemu za mji wa Kilifi katika kaunti ya Kilifi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za kisiwa cha Lamu katika kaunti ya Lamu pia zitashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.

Wakati huohuo, sehemu kadhaa za maeneo ya Hola na Masalani katika kaunti ya Tana River pia zitakumbwa na kukatizwa kwa umeme.