Ruto amfariji mbunge wa Navakholo Wangwe baada ya kifo cha mamake

Mbunge huyo anawakilisha Eneobunge la Navakholo na ni mwanachama wa Chama cha ODM.

Muhtasari
  • "Mawazo na sala zetu ziko pamoja na familia na marafiki katika wakati huu wa huzuni. Rest In Peace."

Rais William Ruto ameifariji familia ya mbunge wa Navakholo Emmanuel Wangwe baada ya kifo cha mamake, Agneta Nerima.

Rais alimsifu kama mkulima wa kiroho na aliyejitolea ambaye aliongoza watu wengi.

"Pole zetu kwa Mheshimiwa Emmanuel Wangwe kwa kuondokewa na mama yake mpendwa Agneta Nerima. Mama Nerima alikuwa wa kiroho na mkulima aliyejitolea ambaye ushauri wake uliwagusa watu wengi," alisema.

"Mawazo na sala zetu ziko pamoja na familia na marafiki katika wakati huu wa huzuni. Rest In Peace."

Mbunge huyo anawakilisha Eneobunge la Navakholo na ni mwanachama wa Chama cha ODM.

Wangwe pia anahudumu kama kinara wa wengi katika Bunge la Kitaifa.