Tazama maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme Jumatatu- KPLC

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Mei 20.

Muhtasari

•KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kunatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

•Baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa tisa alasiri.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Mei 20.

Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kunatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Kampuni ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa tisa alasiri.Kaunti ambazo zitaathirika ni Nyeri na Kiambu.

Katika kaunti ya Kiambu, baadhi ya sehemu za maeneo ya Kagwe, Pascha, na Githunguri ndizo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni siku ya Jumatatu.

Sehemu kadhaa zilizozingira soko la Giakaibei katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Sehemu hizo ni pamoja na soko la Giakaibei, Shule ya upili ya Giakaibei, Shule ya upili ya Kanjuri, soko la Kanjuri, Kiunjugi TBC, Kariambi TBC, Gitima, Ragati miongoni mwa zingine.