Matokeo ya KUCCPS : Fahamu jinsi unaweza kuangalia Chuo Kikuu ambacho umeitwa

Wanafunzi waliochaguliwa wanatarajiwa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali kuanzia Septemba mwaka huu.

Muhtasari

•KUCCPS imewaalika rasmi wanafunzi katika vyuo vikuu mbalimbali vya umma na vya kibinafsi kote nchini.

•Waombaji sasa wanaweza kuangalia matokeo ya maombi yao ya shahada au diploma kwenye tovuti rasmi ya KUCCPS.

ametoa rasmi ripoti ya KUCCPS YA 2024/25.
Waziri Ezekiel Machogu ametoa rasmi ripoti ya KUCCPS YA 2024/25.
Image: MAKTABA

Huduma ya Kupanga Wanafunzi katika Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kenya (KUCCPS) imewaalika rasmi wanafunzi katika vyuo vikuu mbalimbali vya umma na vya kibinafsi kote nchini.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alitoa rasmi ripoti ya Upangaji wa KUCCP'S 2024/2025 wa Wanafunzi katika vyuo vikuu na vyuo mnamo siku ya Jumatano, Mei 21 katika The Edge Convention Centre- College of Insurance mtaani South C, Nairobi.

Mwenyekiti wa Bodi ya KUCCPS, Bw Cyrus Gituai, na Mkurugenzi Mtendaji Dkt Agnes Mercy Wahome pia walikuwepo wakati wa kutolewa kwa ripoti hiyo.

Wakati wa hafla hiyo, ilibainika kuwa 85% ya watahiniwa wa KCSE 2023 waliopata  C+ na zaidi walifanya maombi ya vyuo ambapo 76.2% walichagua kozi za digrii huku wengine (11,991) wakichagua Diploma. Shahada ya Elimu ilivutia idadi kubwa zaidi ya waombaji.

Waombaji wa kiume waliendelea kutawala upangaji wa programu za Shahada huku wanafunzi wa kike wakiwa wengi wa wale waliowekwa katika programu za TVET.

Waombaji sasa wanaweza kuangalia matokeo ya maombi yao ya shahada au diploma kwenye tovuti rasmi ya KUCCPS ( https://students.kuccps.net/ ) ambayo tayari imesasishwa.

Wanafunzi waliochaguliwa wanatarajiwa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali kuanzia Septemba mwaka huu.