KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo Alhamisi

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Mei 23.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na   Nairobi, Nakuru, Kisumu, Kakamega, na Kiambu.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Mei 23.

Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na   Nairobi, Nakuru, Kisumu, Kakamega, na Kiambu.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za mtaa wa Garden Estate zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo na Majani Mingi na Testai katika kaunti ya Nakuru zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za eneo la Nyamasaria katika kaunti ya Kisumu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kakamega, baadhi ya sehemu za maeneo ya Kambi Mwanza na Shamberere zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Juja Mukinyi Road zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.