Idadi ya watu walionyongwa yaongezeka kwa 31% duniani, yasema Amnesty International

Shirika hilo lilinakili visa 1,153 vya vya utekelezaji wa adhabu ya kunyongwa mwaka 2023.

Muhtasari

•Mwaka wa 2023, Amnesty International ilinakili idadi ya juu zaidi tangu 2015, wakati watu 1,634 walinyongwa.

•Amnesty pia iligundua kuwa hukumu za kifo zilizotolewa ulimwenguni kote ziliongezeka kwa 20% mnamo 2023.

Kitanzi
Kitanzi
Image: HISANI

Idadi ya adhabu ya kifo inaongezeka duniani kote, kulingana na takwimu za hivi punde kutoka Amnesty International.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu lilinakili visa 1,153 vya vya utekelezaji wa adhabu ya kunyongwa mwaka 2023, ongezeko la asilimia 31 kutoka 883 mwaka 2022. Ni idadi ya juu zaidi kunakiliwa na Amnesty International tangu 2015, wakati watu 1,634 walinyongwa.

Katibu Mkuu wa Amnesty International Agnès Callamard anasema: "Visa vingi vya mauaji vilirekodiwa nchini Iran. Mamlaka ya Iran ilionyesha kutojali kabisa maisha ya binadamu na kuongeza adhabu ya kunyongwa kwa makosa yanayohusiana na dawa za kulevya, na kuangazia zaidi athari za kibaguzi za hukumu ya kifo kwa jamii zilizotengwa na masikini zaidi za Iran.

Ingawa ripoti inaonyesha Iran inahusika na mauaji mengi yaliyorekodiwa, huku watu wasiopungua 853 wakiuawa, Amnesty inaamini kuwa China ndiyo nchi iliyo na watu wengi zaidi kunyongwa.

Hakuna takwimu rasmi kutoka China kuhusu idadi ya walionyongwa, lakini Amnesty inakadiria kuwa maelfu ya watu waliuawa nchini humo mwaka jana.

Amnesty pia iligundua kuwa hukumu za kifo zilizotolewa ulimwenguni kote ziliongezeka kwa 20% mnamo 2023.

Ni idadi kubwa zaidi ya adhabu za kifo zilizotolewa tangu 2018.

Ni nchi gani yanatekeleza adhabu ya kifo zaidi?

Image: BBC

Amnesty inasema nchi tano zilizokuwa na idadi kubwa ya watu walionyongwa mwaka 2023 ni China, Iran, Saudi Arabia, Somalia na Marekani. Iran pekee ilichangia 74% ya watu wote walionyongwa, huku Saudi Arabia ikiwa na 15%.

Sawa na China Amnesty inasema haikuweza kupata takwimu rasmi kutoka Korea Kaskazini, Vietnam, Syria, maeneo ya Palestina na Afghanistan.

Image: BBC

Je, ni nchi ngapi zimefuta hukumu ya kifo?

Idadi ya nchi ambazo zimeondoa hukumu ya kifo imeongezeka kutoka 48 mwaka 1991 hadi 112 mwaka 2023.

Nchi 9 zinaitumia kwa uhalifu mbaya zaidi, wakati nchi 23 ambazo zina hukumu ya kifo hazijatumia adhabu ya kifo kwa angalau muongo mmoja.

Je, nchi hutekeleza vipi hukumu ya kifo?

Kuna njia nne zilitumika kutekeleleza adhabu ya kifu mwaka 2023, huku ukataji wa kichwa ukitumika nchini Saudi Arabia pekee.

Nchi saba zilitumia kamba kunyonga, watu sita waliuawa kwa kupigwa risasi na watatu walichomwa sindano za kuua mwaka jana.

Image: BBC

Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk anasema : “Kutolewa kwa hukumu ya kifo ni vigumu sana kulinganisha na utu wa binadamu, haki ya msingi ya kuishi, na haki ya kuishi bila mateso au ukatili, kutendewa unyama au kudhalilisha. ”

Kuondolewa hatia

Mtu huondolewa hatia, baada ya hukumu kutolewa na mchakato wa rufaa kuhitimishwa. Mtu aliyetiwa hatiani baadaye anaondolewa lawama au kuachiliwa kwa shtaka la jinai, na kwa hiyo anachukuliwa kuwa hana hatia mbele ya sheria.

Amnesty International ilirekodi msamaha 9 wa wafungwa wanaokabiliwa na hukumu za kifo katika nchi tatu: Kenya (5), Marekani (3), Zimbabwe (1).

Wanaharakati wa haki za binadamu wanapinga hukumu ya kifo ili kuzuia watu kupatikana bila hatia baada ya kunyongwa.

Kuzuia

Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kwamba nchi ambazo zina adhabu ya kifo kwa kiasi kikubwa huidumisha "kwa sababu mtazamo kwamba inazuia uhalifu".

Makubaliano kati ya wanasayansi wa kijamii ni kwamba athari ya kuzuia hukumu ya kifo haijathibitishwa.

Wengine wanasema kinachozuia zaidi ni uwezekano wa kukamatwa na kuadhibiwa.

Mnamo 1988, Umoja wa Mataifa ulifanya uchunguzi ili kubaini uhusiano kati ya viwango vya hukumu ya kifo na mauaji. Matokeo yalitolewa mwaka wa 1996. Yalisema hivi: “Uchunguzi umeshindwa kutoa uthibitisho wa kisayansi kwamba kunyongwa kuna athari kubwa zaidi kuliko kifungo cha maisha.”

Maelezo ya picha,The US uses death chambers to execute prisoners after a term on death row

Athari kwa watoto

Mnamo mwaka 2010, nchi 14, zikiwemo Algeria, Argentina, Kazakhstan, Mexico na Uturuki zilikuja pamoja na kuanzisha Tume ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo.

Tume imekua na nchi wanachama 24, zikiwemo Uingereza, Canada, Australia, Ujerumani na Togo.

Katika ripoti yake ya hivi punde, iliyotolewa mwaka jana, Tume hiyo ilisisitiza kuwa watoto wako katika hatari ya kunyongwa katika nchi nyingi licha ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto kupiga marufuku mwenendo huo. Mkataba huo unatumika katika nchi 196.

Chama cha Wanasaikolojia wa Marekani (APA) kinatoa wito kwa mataifa ya Marekani kuzuia matumizi ya hukumu ya kifo dhidi ya mtu yeyote aliye na umri wa chini ya miaka 21.

Inasema hivi: “Kulingana na hali ya sasa ya sayansi, akili za watoto wenye umri wa miaka 18 hadi 20 haziwezi kusemwa kuwa tofauti sana na zile za watoto wenye umri wa miaka 17.”

Inaendelea kusema: “Sifa zilezile za ujana na kutokomaa ambazo huhalalisha kutotoa hukumu ya kifo kwa wenye umri wa miaka 16 na 17 zipo kwa wenye umri wa miaka 18 hadi 20.”

Watoto hawaathiriwi tu na kunyongwa. "Tofauti na aina nyingine za adhabu kwa mhalifu, kunyongwa kwa mzazi kunamnyima mtoto nafasi ya kuwa na uhusiano na mzazi wake," inasema Tume.