Tazama maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Alhamisi- KPLC

baadhi ya maeneo ya kaunti tano yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Muhtasari

•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kunatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, , Nyeri, Tharaka Nithi Kiambu na Mombasa.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Mei 30.

Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kunatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Kampuni ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na  moja jioni.Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, , Nyeri, Tharaka Nithi Kiambu na Mombasa.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za mtaa wa Utawala zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Wamagana na Mbaaini katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kiraro na Kianjagi  katika kaunti ya Tharaka Nithi pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Katika kaunti ya Kiambu, sehemu kadhaa za maeneo ya Ndula, Kolping, Nyacaba, Maraba, Ondiri, Karai, Riabai, na Migaa zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, baadhi ya sehemu za maeneo ya Miritini, Bonje, na Mazeras katika kaunti ya Mombasa pia zitaathirika.