Wezi wamvamia afisa mkuu wa polisi akiwa amelala na kumpiga, kumuibia pesa na runinga

Mkuu huyo wa polisi kitengo cha Superitendent alivamiwa na kundi hilo la vijana wenye silaha nyumbani kwake majira ya saa tisa alfajiri akiwa amelala na kumpiga vibaya kabla ya kutoroka na mfuko wa hela na runinga.

Muhtasari

• Jarida hilo linaripoti kwamba tayari vijana 4 wamekamatwa kutokana na tukio hilo lililojiri Jumanne.

Mwanamke mjamzito apatikana amedungwa visu mgongoni
Mwanamke mjamzito apatikana amedungwa visu mgongoni
Image: Maktaba//The Star

Vitengo vya polisi nchini Uganda vimeanzisha uchunguzi kubaini wahusika katika tukio ambalo afisa mkuu wa polisi alivamiwa na genge la watu waliokuwa wamejihami nyakati za usiku akiwa amelala kabla ya kumshambulia na kumuibia mfuko wa pesa na runinga na kutokomea gizani.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, mkuu huyo wa polisi kitengo cha Superitendent alivamiwa na kundi hilo la vijana wenye silaha nyumbani kwake majira ya saa tisa alfajiri akiwa amelala na kumpiga vibaya kabla ya kutoroka na mfuko wa hela na runinga.

Jarida hilo linaripoti kwamba tayari vijana 4 wamekamatwa kutokana na tukio hilo lililojiri Jumanne.

“Wahuni hao walipata njia ya kuingia nyumbani kwa afisa wa polisi wakati akiwa amelala. Waliiba runinga ya kisasa yenye thamani ya shilingi milioni 1.2 [Za Uganda], mfuko wa begi uliokuwa na kiasi cha hela kisichokadirika kwa sasa kabla ya kumtia majeraha mabaya. Wezi hao baadae walitoroka kutoka kwa eneo la tukio,” jarida hilo lilimnukuu polisi anayesimamia uchunguzi huo.

Kwa sasa, washukiwa wanne wanaodaiwa kuhusika na shambulizi hilo wamekamatwa na mamlaka, huku juhudi zikiendelea za kurejesha mali iliyoibwa.

"Kwa msaada wa kitengo cha mbwa, wapelelezi wetu waliweza kuwasaka washukiwa. Bado hawajafichua walikoweka vitu vilivyoibiwa. Hilo sasa ndilo lengo letu," aliongeza.

Afisa huyo aliyevamiwa kwa sasa anaripotiwa kuwa katika hali nzuri akipokea matibabu hospitalini.