Maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Ijumaa- KPLC

baadhi ya maeneo ya kaunti nne yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Muhtasari

•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kunatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
•Kaunti ambazo zitaathirika ni Makueni, West Pokot, Nyeri,na Mombasa.

Kenya Power
Image: HISANI

Kampuni ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Mei 31.

Katika taarifa ya Alhamisi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kunatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Kampuni ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na  moja jioni.Kaunti ambazo zitaathirika ni Makueni, Nyeri,Mombasa na West Pokot .

Katika kaunti ya Makueni, sehemu kadhaa kama Sultan Town, Sultan Police, Holy Ghost Schools, Kalimbini, Ngokomi, Kwothithu, Kiongwani, Kima, Kiu, Salama, Kautandini, Malili, Enzai, Nunguni, Kilungu, Kavatanzou, Mitini, Kyambekezitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Chorong'i C/Fact, Kiamwathi Market,katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Mjini Mombasa, sehemu ambazo zitaathirika ni  Shule ya Upili ya Shimo Latewa, Mama Ngina Girls, Flamingo Hotel, Serena Residences, Mtwapa Town, Mtoondoni, Mtepeteni na wateja walio karibu.

Maeneo ya Pokot Magharibi ambayo yataathiriwa ni pamoja na Siyoi, Kaibos, Paraiywa, Kabichbich, Kipat, Kapsait, Kaptabuk, Kokwoplekwa, Kapsangar na wateja walio karibu.